Isaya 48:7 - Swahili Revised Union Version Yameumbwa sasa, wala si tokea zamani; na kabla ya siku hii ya leo hukusikia habari yake; usije ukasema, Tazama, niliyajua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mambo hayo yanatukia sasa; hukupata kuyasikia kabla ya leo, hivyo huwezi kusema, ‘Aa! Nilikwisha yajua.’ Biblia Habari Njema - BHND Mambo hayo yanatukia sasa; hukupata kuyasikia kabla ya leo, hivyo huwezi kusema, ‘Aa! Nilikwisha yajua.’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mambo hayo yanatukia sasa; hukupata kuyasikia kabla ya leo, hivyo huwezi kusema, ‘Aa! Nilikwisha yajua.’ Neno: Bibilia Takatifu Yameumbwa sasa, wala si tangu zamani; hukupata kuyasikia kabla ya siku ya leo. Hivyo huwezi kusema, ‘Naam, niliyajua hayo.’ Neno: Maandiko Matakatifu Yameumbwa sasa, wala si tangu zamani; hukupata kuyasikia kabla ya siku ya leo. Hivyo huwezi kusema, ‘Naam, niliyajua hayo.’ BIBLIA KISWAHILI Yameumbwa sasa, wala si tokea zamani; na kabla ya siku hii ya leo hukusikia habari yake; usije ukasema, Tazama, niliyajua. |
Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua.
Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nilijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;
BWANA, mkombozi wa Israeli, Mtakatifu wake, amwambia hivi yeye anayedharauliwa na wanadamu; yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao; Wafalme wataona, watasimama; wakuu nao watasujudu; kwa sababu ya BWANA aliye mwaminifu, Mtakatifu wa Israeli aliyekuchagua.