BWANA, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni.
Isaya 45:10 - Swahili Revised Union Version Ole wake amwambiaye baba yake, Wazaa nini? Au mwanamke, Una uchungu wa kujifungua nini? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ole wake mtoto amwambiaye baba yake, “Kwa nini umenizaa?” Au amwambiaye mama yake, “Ya nini umenileta duniani?” Biblia Habari Njema - BHND Ole wake mtoto amwambiaye baba yake, “Kwa nini umenizaa?” Au amwambiaye mama yake, “Ya nini umenileta duniani?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ole wake mtoto amwambiaye baba yake, “Kwa nini umenizaa?” Au amwambiaye mama yake, “Ya nini umenileta duniani?” Neno: Bibilia Takatifu Ole wake amwambiaye baba yake, ‘Umezaa nini?’ Au kumwambia mama yake, ‘Umezaa kitu gani?’ Neno: Maandiko Matakatifu Ole wake amwambiaye baba yake, ‘Umezaa nini?’ Au kumwambia mama yake, ‘Umezaa kitu gani?’ BIBLIA KISWAHILI Ole wake amwambiaye baba yake, Wazaa nini? Au mwanamke, Una uchungu wa kujifungua nini? |
BWANA, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni.
Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unatengeneza nini? Au chombo ulichotengeneza hakina mikono?
Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?
Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawaheshimu; basi si ni afadhali zaidi kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?