Yakumbukeni matendo yake yote ya ajabu aliyoyafanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
Isaya 43:18 - Swahili Revised Union Version Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ‘Msiyanganganie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani. Biblia Habari Njema - BHND ‘Msiyanganganie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ‘Msiyang'ang'anie mambo yaliyopita, wala msifikirie vitu vya zamani. Neno: Bibilia Takatifu “Msiyakumbuke mambo yaliyopita, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Neno: Maandiko Matakatifu “Msiyakumbuke mambo yaliyopita, wala msiyatafakari mambo ya zamani. BIBLIA KISWAHILI Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. |
Yakumbukeni matendo yake yote ya ajabu aliyoyafanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;
Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.
Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.