Isaya 14:8 - Swahili Revised Union Version Naam, misonobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Misonobari inafurahia kuanguka kwako, nayo mierezi ya Lebanoni pamoja yasema: ‘Kwa vile sasa umeangushwa, hakuna mkata miti atakayekuja dhidi yetu!’ Biblia Habari Njema - BHND Misonobari inafurahia kuanguka kwako, nayo mierezi ya Lebanoni pamoja yasema: ‘Kwa vile sasa umeangushwa, hakuna mkata miti atakayekuja dhidi yetu!’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Misonobari inafurahia kuanguka kwako, nayo mierezi ya Lebanoni pamoja yasema: ‘Kwa vile sasa umeangushwa, hakuna mkata miti atakayekuja dhidi yetu!’ Neno: Bibilia Takatifu Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni inashangilia mbele yako na kusema, “Basi kwa kuwa umeangushwa chini, hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.” Neno: Maandiko Matakatifu Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni inashangilia mbele yako na kusema, “Basi kwa sababu umeangushwa chini, hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.” BIBLIA KISWAHILI Naam, misonobari inakufurahia, Na mierezi ya Lebanoni, ikisema, Tokea wakati ulipolazwa chini wewe, Hapana mkata miti aliyetujia. |
Umemshutumu Bwana kwa watumishi wako, kwa kuwa umesema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani ya Lebanoni; nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misonobari yake mizuri, nami nitaingia ndani ya mahali pake palipoinuka, palipo mbali sana, msitu wa shamba lake lizaalo sana.
Niliwatetemesha mataifa kwa mshindo wa kuanguka kwake, hapo nilipomtupa chini mpaka kuzimu, pamoja nao washukao shimoni; na miti yote ya Adeni, miti iliyo miteule na iliyo mizuri ya Lebanoni, yote inywayo maji, ilifarijika pande za chini za nchi.
Piga yowe, msonobari, maana mwerezi umeanguka, Kwa sababu miti iliyo mizuri imeharibika; Pigeni yowe, enyi mialoni ya Bashani, Kwa maana msitu wenye nguvu umeangamia.