Isaya 14:11 - Swahili Revised Union Version Fahari yako imeshushwa hadi kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Fahari yako imeteremshwa kuzimu pamoja na muziki wa vinubi vyako. Chini mabuu ndio kitanda chako, na wadudu ndio blanketi lako!’ Biblia Habari Njema - BHND Fahari yako imeteremshwa kuzimu pamoja na muziki wa vinubi vyako. Chini mabuu ndio kitanda chako, na wadudu ndio blanketi lako!’ Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Fahari yako imeteremshwa kuzimu pamoja na muziki wa vinubi vyako. Chini mabuu ndio kitanda chako, na wadudu ndio blanketi lako!’ Neno: Bibilia Takatifu Majivuno yako yote yameshushwa hadi Kuzimu, pamoja na kelele ya vinubi vyako, mafunza yametanda chini yako, na minyoo imekufunika. Neno: Maandiko Matakatifu Majivuno yako yote yameshushwa mpaka kuzimu, pamoja na kelele ya vinubi vyako, mafunza yametanda chini yako, na minyoo imekufunika. BIBLIA KISWAHILI Fahari yako imeshushwa hadi kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. |
Ewe uliyejaa makelele, Mji wa ghasia, mji wenye furaha; Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga, Wala hawakufa vitani.
Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo.
Maana nondo atawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote.
Nao watatoka nje na kuitazama mizoga ya watu walioniasi; maana funza wao hatakufa, wala moto wao hautazimika nao watakuwa chukizo machoni pa wote wenye mwili.