Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?
Hosea 9:5 - Swahili Revised Union Version Mtafanya nini katika siku ya mkutano wa sikukuu teule, na katika siku ya karamu ya BWANA? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtafanya nini katika sikukuu ile iliyopangwa, au katika karamu ya Mwenyezi-Mungu? Biblia Habari Njema - BHND Mtafanya nini katika sikukuu ile iliyopangwa, au katika karamu ya Mwenyezi-Mungu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtafanya nini katika sikukuu ile iliyopangwa, au katika karamu ya Mwenyezi-Mungu? Neno: Bibilia Takatifu Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa, katika siku za sikukuu za Mwenyezi Mungu? Neno: Maandiko Matakatifu Mtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa, katika siku za sikukuu za bwana? BIBLIA KISWAHILI Mtafanya nini katika siku ya mkutano wa sikukuu teule, na katika siku ya karamu ya BWANA? |
Nanyi mtafanya nini siku ya kujiliwa, na wakati wa uangamivu, utakaokuja kutoka mbali sana? Je! Mtamkimbilia nani mpate msaada? Na utukufu wenu mtauacha wapi?
Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?
Tena nitaikomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na makusanyiko yake yote yaliyoamriwa.
Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njooni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.