Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Hesabu 5:29 - Swahili Revised Union Version

Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

“Basi, hii ndiyo sheria kuhusu kesi za wivu iwapo mwanamke, ingawa yu chini ya mamlaka ya mumewe, atapotoka na kujitia unajisi,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

“Basi, hii ndiyo sheria kuhusu kesi za wivu iwapo mwanamke, ingawa yu chini ya mamlaka ya mumewe, atapotoka na kujitia unajisi,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

“Basi, hii ndiyo sheria kuhusu kesi za wivu iwapo mwanamke, ingawa yu chini ya mamlaka ya mumewe, atapotoka na kujitia unajisi,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

“ ‘Basi, hii ndiyo sheria ya wivu mwanamke anapopotoka na kujitia unajisi akiwa ameolewa na mumewe,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

“ ‘Basi, hii ndiyo sheria ya wivu mwanamke anapopotoka na kujitia unajisi akiwa ameolewa na mumewe,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi;

Tazama sura
Tafsiri zingine

Hesabu 5:29
12 Marejeleo ya Msalaba  

Mnategemea upanga wenu, mnatenda machukizo, kila mmoja wenu anamnajisi mke wa jirani yake; je! Mtaimiliki nchi hii?

Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi;

Na katika pigo la ukoma katika vazi la sufu, au la kitani, kama ni katika lililofumwa, au lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi, sheria yake ni hiyo, kusema kwamba ni safi, au kusema kwamba ni najisi.

Na sheria ya matoleo ya sadaka za amani, atakazosongeza mtu kwa BWANA, ni hii.

Nena na wana wa Israeli, uwaambie, kama mke wa mtu yeyote akikengeuka, na kumkosa mumewe,

ndipo huyo mume atamchukua mkewe, aende naye kwa kuhani, naye ataleta sadaka yake kwa ajili yake, yaani, sehemu ya kumi ya efa; asitie mafuta juu yake, wala asitie ubani juu yake; maana, ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho ya kukumbukia uovu.

tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena ikiwa hukukengeuka kutenda maovu, ukiwa chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana yasikudhuru;

Na kama mwanamke hakuwa na unajisi lakini yu safi; ndipo ataachiliwa, naye atazaa wana.

au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume, naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za BWANA, na kuhani atatenda juu yake sheria hii yote.