Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Hesabu 36:4 - Swahili Revised Union Version Tena itakapokuwapo hiyo jubilii ya wana wa Israeli, ndipo urithi wa hilo kabila ambalo wamekuwa ndani yake utaongezewa huo urithi wao; hivyo urithi wao utaondolewa katika urithi wa kabila la baba zetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Katika sikukuu ya ukumbusho urithi wao utahesabiwa pamoja na ule wa kabila watakamoolewa na hivyo kabila letu halitapata urithi huo tena.” Biblia Habari Njema - BHND Katika sikukuu ya ukumbusho urithi wao utahesabiwa pamoja na ule wa kabila watakamoolewa na hivyo kabila letu halitapata urithi huo tena.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Katika sikukuu ya ukumbusho urithi wao utahesabiwa pamoja na ule wa kabila watakamoolewa na hivyo kabila letu halitapata urithi huo tena.” Neno: Bibilia Takatifu Mwaka wa Yubile kwa Waisraeli utakapofika, urithi wao utaongezwa kwa lile kabila ambalo wameolewa, na mali yao itaondolewa kutoka urithi wa kabila la mababu zetu.” Neno: Maandiko Matakatifu Wakati mwaka wa Yubile kwa Waisraeli utafika, urithi wao utaongezwa kwa lile kabila ambalo wameolewa, na mali yao itaondolewa kutoka urithi wa kabila la mababu zetu.” BIBLIA KISWAHILI Tena itakapokuwapo hiyo jubilii ya wana wa Israeli, ndipo urithi wa hilo kabila ambalo wamekuwa ndani yake utaongezewa huo urithi wao; hivyo urithi wao utaondolewa katika urithi wa kabila la baba zetu. |
Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wapangaji wangu.
Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arubaini na tisa.
Wakiolewa na watu wa wana wa hayo makabila mengine ya wana wa Israeli, ndipo urithi wao utatwaliwa na kuondolewa katika urithi wa baba zetu, na hilo kabila watakalotiwa ndani yake litaongezewa urithi wao; basi urithi huo utaondolewa katika kura ya urithi wetu.
Basi Musa akawaagiza wana wa Israeli kama neno la BWANA lilivyokuwa, akasema, Kabila la wana wa Yusufu imenena yaliyo haki.