Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua;
Hesabu 27:22 - Swahili Revised Union Version Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru; akamtwaa Yoshua, akamweka mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya jumuiya yote; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Alimtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na jumuiya yote ya Waisraeli. Biblia Habari Njema - BHND Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Alimtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na jumuiya yote ya Waisraeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mose akafanya kama alivyoamriwa na Mwenyezi-Mungu. Alimtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na jumuiya yote ya Waisraeli. Neno: Bibilia Takatifu Musa akafanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza. Akamtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na kusanyiko lote. Neno: Maandiko Matakatifu Musa akafanya kama bwana alivyomwagiza. Akamtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na kusanyiko lote. BIBLIA KISWAHILI Musa akafanya kama BWANA alivyomwamuru; akamtwaa Yoshua, akamweka mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya jumuiya yote; |
Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua;
Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za BWANA; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja naye, mkutano wote pia.
kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama BWANA alivyosema kwa mkono wa Musa.