Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba.
Hesabu 20:26 - Swahili Revised Union Version umvue Haruni mavazi yake, ukamvike Eleazari mwanawe mavazi hayo; kisha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, mvue Aroni mavazi yake rasmi, umvalishe mwanawe Eleazari. Aroni atakufa akiwa huko mlimani.” Biblia Habari Njema - BHND Kisha, mvue Aroni mavazi yake rasmi, umvalishe mwanawe Eleazari. Aroni atakufa akiwa huko mlimani.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, mvue Aroni mavazi yake rasmi, umvalishe mwanawe Eleazari. Aroni atakufa akiwa huko mlimani.” Neno: Bibilia Takatifu Mvue Haruni mavazi yake, na umvike Eleazari mwanawe, kwa maana Haruni atakusanywa pamoja na watu wake; atakufa huko.” Neno: Maandiko Matakatifu Mvue Haruni mavazi yake, na umvike Eleazari mwanawe, kwa maana Haruni atakusanywa pamoja na watu wake; atakufa huko.” BIBLIA KISWAHILI umvue Haruni mavazi yake, ukamvike Eleazari mwanawe mavazi hayo; kisha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko. |
Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba.
Musa akafanya kama BWANA alivyomwagiza; wakakwea katika mlima wa Hori mbele ya macho ya mkutano wote.
Walipizie kisasi wana wa Israeli juu ya Wamidiani; kisha baadaye utakusanywa uwe pamoja na watu wako.
Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine awepo, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?