Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu;
Hesabu 20:21 - Swahili Revised Union Version Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hiyo Israeli akageuka na kumwacha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Waedomu wakakataa kuwapa ruhusa Waisraeli kupita katika mipaka yao. Waisraeli wakageuka na kushika njia nyingine. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Waedomu wakakataa kuwapa ruhusa Waisraeli kupita katika mipaka yao. Waisraeli wakageuka na kushika njia nyingine. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Waedomu wakakataa kuwapa ruhusa Waisraeli kupita katika mipaka yao. Waisraeli wakageuka na kushika njia nyingine. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa Waedomu waliwakatalia Waisraeli kupita katika nchi yao, Israeli wakageuka, wakawaacha. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa Waedomu waliwakatalia Waisraeli kupita katika nchi yao, Israeli wakageuka, wakawaacha. BIBLIA KISWAHILI Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hiyo Israeli akageuka na kumwacha. |
Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu;
Lakini Sihoni hakukubali kumwacha Israeli kupita katika mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, akatoka aende kupigana na Israeli jangwani, akafika mpaka Yahasa; akapigana na Israeli.
Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia.
Nipishe katikati ya nchi yako; nitakwenda kwa njia ya barabara, sitageuka kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto.
kama walivyonifanyia hao wana wa Esau waishio Seiri, na hao Wamoabi waishio Ari; hata nivuke Yordani niingie nchi tupewayo na BWANA, Mungu wetu.
Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake.
ndipo Israeli wakatuma wajumbe waende kwa mfalme wa Edomu, wakisema, Nakuomba sana unipe ruhusa nipite katika nchi yako; lakini mfalme wa Edomu hangewasikiliza. Pia waliwatuma wajumbe kwa mfalme wa Moabu; wala naye hakukubali; basi Israeli wakakaa katika Kadeshi.
Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki mwa nchi ya Moabu, wakapiga kambi upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.
Je! Wewe hutakitamalaki hicho ambacho huyo Kemoshi mungu wako akupa kukitamalaki? Kadhalika si sisi ndio watu wa kutamalaki vyote ambavyo BWANA, Mungu wetu ametwaa kwa manufaa yetu?