Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi.
ndipo kuhani ataagiza kwamba watoe vyote vilivyomo nyumbani, kabla kuhani hajaingia ndani kuliangalia hilo pigo, ili vyote vilivyomo nyumbani visiwe najisi, kisha baadaye kuhani ataingia ndani ya nyumba hiyo aikague;