Hesabu 13:8 - Swahili Revised Union Version Katika kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni. Biblia Habari Njema - BHND Kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni. Neno: Bibilia Takatifu kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni; Neno: Maandiko Matakatifu kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni; BIBLIA KISWAHILI Katika kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni |
Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, Kuna kelele ya vita kambini.
Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa tangu ujana wake, akajibu akasema, Ee bwana wangu Musa, uwakataze.
Hayo ndiyo majina ya hao watu waliotumwa na Musa waende kuipeleleza nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita jina lake Yoshua.
BWANA akamwambia Musa, Tazama, siku zako za kufa zinakaribia, umwite Yoshua, nanyi mkajihudhurishe katika hema ya kukutania, ili nipate kumwagiza kazi. Musa na Yoshua wakaenda, wakajihudhurisha ndani ya hema ya kukutania.
Akamwagiza Yoshua, mwana wa Nuni, akamwambia, Uwe hodari na moyo mkuu, kwa kuwa utawapeleka wana wa Israeli katika nchi niliyowaapia; nami nitakuwa pamoja nawe.
Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni.
Na Yoshua, mwana wa Nuni, alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake; wana wa Israeli wakamsikiliza, wakafanya kama BWANA alivyomwamuru Musa.
Wakamjibu Yoshua, wakasema, Hayo yote uliyotuamuru tutayafanya, na kila mahali utakakotutuma tutakwenda.
kulingana na ile amri ya BWANA wakampa mji alioutaka, maana, ni Timnath-sera katika nchi ya vilima ya Efraimu; naye akaujenga huo mji na kukaa mumo.