Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
Hesabu 11:14 - Swahili Revised Union Version Mimi siwezi kuwawaongoza watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo mzito sana wa kunishinda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siwezi kuwatunza watu wote hawa peke yangu; hilo ni jukumu kubwa mno kwangu! Biblia Habari Njema - BHND Siwezi kuwatunza watu wote hawa peke yangu; hilo ni jukumu kubwa mno kwangu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siwezi kuwatunza watu wote hawa peke yangu; hilo ni jukumu kubwa mno kwangu! Neno: Bibilia Takatifu Mimi siwezi kuwabeba watu hawa wote peke yangu, mzigo ni mzito sana kwangu. Neno: Maandiko Matakatifu Mimi siwezi kuwabeba watu hawa wote peke yangu, mzigo ni mzito sana kwangu. BIBLIA KISWAHILI Mimi siwezi kuwaongoza watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo mzito sana wa kunishinda. |
Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
Kwa kweli utajidhoofisha mwenyewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako.
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atakuwa na heshima ya kifalme; na ataketi na kutawala; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na maelewano yenye amani yatakuwa kati ya hao wawili.
katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?