Filemoni 1:21 - Swahili Revised Union Version Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba. Biblia Habari Njema - BHND Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba. Neno: Bibilia Takatifu Huku nikiwa na hakika ya kutii kwako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba. Neno: Maandiko Matakatifu Nikiwa na hakika ya utii wako, nakuandikia, nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya yale ninayokuomba. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo. |
Nami niliwaandikia neno lilo hilo, ili nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumaini ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.
Nasi pamoja nao tumemtuma ndugu yetu tuliyemwona mara nyingi kuwa ana bidii katika mambo mengi, na sasa ana bidii zaidi sana kwa sababu ya tumaini kuu alilo nalo kwenu.
Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewasumbua atachukua hukumu yake, awaye yote.
Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza na kwamba mtaendelea kuyafanya.