Ndipo mfalme akatuma majibu; Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika.
Ezra 4:18 - Swahili Revised Union Version Ule barua mliotutumia umesomwa wazi mbele yangu, nami nikaielewa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Barua mliyonitumia imetafsiriwa na kusomwa mbele yangu. Biblia Habari Njema - BHND “Barua mliyonitumia imetafsiriwa na kusomwa mbele yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Barua mliyonitumia imetafsiriwa na kusomwa mbele yangu. Neno: Bibilia Takatifu Barua mliyotutumia imesomwa na kutafsiriwa mbele yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Barua mliyotutumia imesomwa na kutafsiriwa mbele yangu. BIBLIA KISWAHILI Ule waraka mliotutumia umesomwa wazi mbele yangu, nami nikauelewa. |
Ndipo mfalme akatuma majibu; Kwa Rehumu, mtawala, na Shimshai, mwandishi, na wenzao wengine waliokaa katika Samaria, na penginepo ng'ambo ya Mto, Salamu; na kadhalika.
Nikatoa amri, na watu wametafuta habari; ikaonekana ya kuwa mji huu zamani umewaasi wafalme, na ya kuwa uasi na fitina zimefanyika ndani yake.
Nao wakasoma katika kitabu, katika Torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa.