Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika miliki yao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.
Ezra 2:43 - Swahili Revised Union Version Wanethini; wazawa wa Siha, wazawa wa Hasufa, wazawa wa Tabaothi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Koo za watumishi wa hekalu waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa: Ukoo wa Siha, wa Hasufa, wa Tabaothi, Biblia Habari Njema - BHND Koo za watumishi wa hekalu waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa: Ukoo wa Siha, wa Hasufa, wa Tabaothi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Koo za watumishi wa hekalu waliorudi kutoka uhamishoni zilikuwa: ukoo wa Siha, wa Hasufa, wa Tabaothi, Neno: Bibilia Takatifu Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, Neno: Maandiko Matakatifu Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, BIBLIA KISWAHILI Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi; |
Basi wenyeji wa kwanza waliokaa katika miliki yao katika miji yao walikuwa Israeli, na makuhani, na Walawi, na Wanethini.
Akina bawabu; wazawa wa Shalumu, wazawa wa Ateri, wazawa wa Talmoni, wazawa wa Akubu, wazawa wa Hatita, wazawa wa Shobai; jumla yao ni mia moja thelathini na tisa.
Wanethini wote, pamoja na wazawa wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.
Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.
Nikawatuma kwa Ido, mkuu, huko Kasifia; nikawaambia watakayomwambia Ido, na ndugu zake hao Wanethini, huko Kasifia, kwamba watuletee watu watakaohudumu katika nyumba ya Mungu wetu.
na katika Wanethini, ambao Daudi, na wakuu, walikuwa wamewaweka kwa ajili ya utumishi wa Walawi, Wanethini mia mbili na ishirini; wote wametajwa kwa majina yao.
Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa Torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;
Basi hawa ndio viongozi wa jimbo waliokaa Yerusalemu; ila mijini mwa Yuda wakakaa kila mtu katika milki yake mijini mwao, yaani, Israeli, makuhani, na Walawi, na Wanethini, wazawa wa watumishi wa Sulemani.
(basi Wanethini hukaa Ofeli), mpaka mahali paelekeapo lango la maji kukabili mashariki, nao mnara utokezao.
Nawe utawapa Haruni na wanawe hao Walawi wawe nao; amepewa watu hao kabisa kwa ajili ya wana wa Israeli.