Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Ezra 2:34 - Swahili Revised Union Version Watu wa Yeriko, mia tatu arubaini na watano. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wa mji wa Yeriko: 345; Biblia Habari Njema - BHND wa mji wa Yeriko: 345; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wa mji wa Yeriko: 345; Neno: Bibilia Takatifu wazao wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano (345); BIBLIA KISWAHILI Watu wa Yeriko, mia tatu arobaini na watano. |
Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Wakaondoka wale watu waliotajwa majina yao, wakawatwaa wafungwa, wakawavika kwa zile nyara wale wote waliokuwa uchi, wakawapa mavazi na viatu, wakawalisha, wakawanywesha, wakawatia mafuta, wakawapandisha waliokuwa dhaifu miongoni mwao juu ya punda wakawaleta Yeriko, mji wa mitende, kwa ndugu zao; kisha wakarudi Samaria.
Sehemu iliyofuata ilijengwa na watu wa Yeriko. Na baada yao Zakuri mwana wa Imri akajenga.