Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona.
Danieli 1:14 - Swahili Revised Union Version Basi akawasikiliza katika jambo hilo, akawajaribu siku kumi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mlinzi akakubaliana nao, akawajaribu kwa muda wa siku kumi. Biblia Habari Njema - BHND Mlinzi akakubaliana nao, akawajaribu kwa muda wa siku kumi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mlinzi akakubaliana nao, akawajaribu kwa muda wa siku kumi. Neno: Bibilia Takatifu Basi akakubali jambo hili, akawajaribu kwa siku kumi. Neno: Maandiko Matakatifu Basi akakubali jambo hili, akawajaribu kwa siku kumi. Swahili Roehl Bible 1937 Akawaitikia neno hili, akawajaribu siku kumi. |
Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona.
Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.
Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.