Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, na kuwa dhihaka kati ya adui zao,
2 Wakorintho 5:3 - Swahili Revised Union Version ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tuko uchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naam, tunapaswa kuvikwa namna hiyo ili tusije tukasimama mbele ya Mungu bila vazi. Biblia Habari Njema - BHND Naam, tunapaswa kuvikwa namna hiyo ili tusije tukasimama mbele ya Mungu bila vazi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naam, tunapaswa kuvikwa namna hiyo ili tusije tukasimama mbele ya Mungu bila vazi. Neno: Bibilia Takatifu kwa kuwa tukishavikwa hatutaonekana tena kuwa uchi. Neno: Maandiko Matakatifu kwa kuwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tena kuwa uchi. BIBLIA KISWAHILI ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tuko uchi. |
Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi, maana Haruni amewaacha waasi, na kuwa dhihaka kati ya adui zao,
Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twapumua kwa shida, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
(Tazama, naja kama mwizi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.