Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.
2 Wafalme 20:16 - Swahili Revised Union Version Isaya akamwambia Hezekia, Basi, lisikie neno la BWANA, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la Mwenyezi-Mungu: Biblia Habari Njema - BHND Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la Mwenyezi-Mungu: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la Mwenyezi-Mungu: Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la Mwenyezi Mungu: Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la bwana: BIBLIA KISWAHILI Isaya akamwambia Hezekia, Basi, lisikie neno la BWANA, |
Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nilimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kulia na wa kushoto.
Ndipo akasema, Wameona nini nyumbani mwako? Hezekia akajibu, Vitu vyote vilivyomo nyumbani mwangu wameviona; hapana kitu nisichowaonesha katika hazina zangu.
Angalia, siku zinakuja, ambazo vitu vyote vilivyomo nyumbani mwako, na hivyo vilivyowekwa akiba na baba zako hata leo, vitachukuliwa mpaka Babeli; hakitasalia kitu, asema BWANA.
Elisha akasema, Lisikieni neno la BWANA; BWANA asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.
Lisikieni neno la BWANA, enyi waamuzi wa Sodoma; tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora.
Basi, sasa lisikie neno la BWANA; Wewe unasema, Usitabiri juu ya Israeli, wala usitoe neno lako juu ya nyumba ya Isaka;
Hata walipokuwa wakishuka kuelekea viunga vya mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atutangulie, naye akitangulia, wewe nawe simama hapa kwa muda, ili nikuambie neno la Mungu.