Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba.
2 Wafalme 12:11 - Swahili Revised Union Version Na fedha iliyopimwa wakawapa mikononi wale waliofanya kazi, walioisimamia nyumba ya BWANA; na hao wakawatolea maseremala na wajenzi walioifanya kazi katika nyumba ya BWANA, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha baada ya kuzipima waliwapa wafanyakazi waliosimamia nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nao wakawalipa maseremala na wajenzi, waliorekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu; Biblia Habari Njema - BHND Kisha baada ya kuzipima waliwapa wafanyakazi waliosimamia nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nao wakawalipa maseremala na wajenzi, waliorekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha baada ya kuzipima waliwapa wafanyakazi waliosimamia nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nao wakawalipa maseremala na wajenzi, waliorekebisha nyumba ya Mwenyezi-Mungu; Neno: Bibilia Takatifu Walipothibitisha kiasi cha hizo fedha, waliwapa watu walioteuliwa kusimamia kazi katika Hekalu. Kwa fedha hizo, wakawalipa wale watu waliofanya kazi katika Hekalu la Mwenyezi Mungu: maseremala na wajenzi, Neno: Maandiko Matakatifu Wakiisha kuthibitisha kiasi cha hizo fedha, waliwapa watu walioteuliwa kusimamia kazi katika Hekalu. Kwa fedha hizo, wakawalipa wale watu waliofanya kazi katika Hekalu la bwana: yaani, maseremala na wajenzi, BIBLIA KISWAHILI Na fedha iliyopimwa wakawapa mikononi wale waliofanya kazi, walioisimamia nyumba ya BWANA; na hao wakawatolea maseremala na wajenzi walioifanya kazi katika nyumba ya BWANA, |
Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba.
Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa BWANA.
na hao waashi, na wakata mawe, tena kununua miti na mawe ya kuchongwa, ili kuyatengeneza mabomoko ya nyumba ya BWANA, tena kwa gharama zote za kuitengeneza nyumba.