Na Waamoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Waamoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari elfu ishirini, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu moja, na watu wa Tobu watu elfu kumi na mbili.
2 Samueli 8:5 - Swahili Revised Union Version Na Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akawapiga watu elfu ishirini na mbili wa Washami. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nao Waaramu wa Damasko walipokwenda kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi aliwashambulia na kuwaua watu 22,000. Biblia Habari Njema - BHND Nao Waaramu wa Damasko walipokwenda kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi aliwashambulia na kuwaua watu 22,000. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nao Waaramu wa Damasko walipokwenda kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi aliwashambulia na kuwaua watu 22,000. Neno: Bibilia Takatifu Waaramu wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua watu elfu ishirini na mbili miongoni mwao. Neno: Maandiko Matakatifu Waaramu wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao. BIBLIA KISWAHILI Na Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akawapiga watu elfu ishirini na mbili wa Washami. |
Na Waamoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Waamoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari elfu ishirini, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu moja, na watu wa Tobu watu elfu kumi na mbili.
Tena Daudi akampiga Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kujipatia tena mamlaka yake huko Mtoni.
Basi Wamisri ni wanadamu wala si Mungu, na farasi wao ni nyama wala si roho; na BWANA atakaponyosha mkono wake, yeye asaidiaye atajikwaa, na yeye asaidiwaye ataanguka, nao wataangamia wote pamoja.
Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila la watu tena;