Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari la jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.
2 Samueli 4:5 - Swahili Revised Union Version Na wale wana wa Rimoni, Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakaenda wakafika nyumbani kwa Ishboshethi, wakati wa joto la mchana, alipokuwa akipumzika adhuhuri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Rekabu na Baana wana wa Rimoni Mbeerothi, wakaenda nyumbani kwa Ishboshethi. Walifika huko adhuhuri, Ishboshethi alipokuwa anapumzika nyumbani kwake. Biblia Habari Njema - BHND Rekabu na Baana wana wa Rimoni Mbeerothi, wakaenda nyumbani kwa Ishboshethi. Walifika huko adhuhuri, Ishboshethi alipokuwa anapumzika nyumbani kwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Rekabu na Baana wana wa Rimoni Mbeerothi, wakaenda nyumbani kwa Ishboshethi. Walifika huko adhuhuri, Ishboshethi alipokuwa anapumzika nyumbani kwake. Neno: Bibilia Takatifu Basi Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi wakaenda nyumbani mwa Ish-Boshethi; walifika huko alipokuwa kwenye mapumziko yake ya mchana. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi wakaenda nyumbani kwa Ish-Boshethi, nao walifika huko wakati alipokuwa kwenye mapumziko yake ya mchana. BIBLIA KISWAHILI Na wale wana wa Rimoni, Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakaenda wakafika nyumbani kwa Ishboshethi, wakati wa joto la mchana, alipokuwa akipumzika adhuhuri. |
Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari la jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.
Basi Abneri, mwana wa Neri, kamanda wa jeshi la Sauli, alikuwa amemtwaa Ishboshethi, mwana wa Sauli, na kumvusha na kumpeleka Mahanaimu;
Na huyo mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili, viongozi wa vikosi; jina lake mmoja akiitwa Baana, na jina la wa pili Rekabu wana wa Rimoni, Mbeerothi, wa wana wa Benyamini; (kwa maana Beerothi umehesabiwa kuwa wa Benyamini;
Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamlia njama; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza;
Hata walipoondoka kwake, (nao walimwacha ameshikwa sana na maradhi,) watumishi wake mwenyewe wakamfanyia fitina kwa ajili ya damu ya mwana wa Yehoyada kuhani, wakamwua kitandani pake, akafa; wakamzika mjini mwa Daudi, lakini hawakumzika katika makaburi ya wafalme.
Basi, toka wakati alipogeuka Amazia katika kumfuata BWANA, wakamfanyia fitina katika Yerusalemu; naye akakimbia mpaka Lakishi; lakini wakatuma kumfuata mpaka Lakishi, wakamwua huko.