Ila Yoabu na Abishai wakamfuatia Abneri; na jua likachwa hapo walipoufikia mlima wa Ama, uelekeao Gia, katika njia ya nyika ya Gibeoni.
2 Samueli 2:25 - Swahili Revised Union Version Nao wana wa Benyamini wakakusanyika pamoja nyuma ya Abneri, wakawa kikosi kimoja, wakasimama juu ya mlima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa kabila la Benyamini wakajikusanya pamoja wakawa nyuma ya Abneri, hivyo wakaunda kikosi chao; nao wakasimama juu ya mlima. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa kabila la Benyamini wakajikusanya pamoja wakawa nyuma ya Abneri, hivyo wakaunda kikosi chao; nao wakasimama juu ya mlima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa kabila la Benyamini wakajikusanya pamoja wakawa nyuma ya Abneri, hivyo wakaunda kikosi chao; nao wakasimama juu ya mlima. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Wabenyamini wakakusanyika tena nyuma ya Abneri. Wakaunda kikosi na kujiimarisha juu ya kilima. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo watu wa kabila la Benyamini wakakusanyika tena nyuma ya Abneri. Wakaunda kikosi na kujiimarisha juu ya kilima. BIBLIA KISWAHILI Nao wana wa Benyamini wakakusanyika pamoja nyuma ya Abneri, wakawa kikosi kimoja, wakasimama juu ya mlima. |
Ila Yoabu na Abishai wakamfuatia Abneri; na jua likachwa hapo walipoufikia mlima wa Ama, uelekeao Gia, katika njia ya nyika ya Gibeoni.
Ndipo huyo Abneri akamwita Yoabu, akasema, Je! Upanga uwale watu sikuzote? Je! Hujui ya kwamba utakuwa uchungu mwisho wake? Basi itakuwa hata lini usijewaamuru watu warudi na kuacha kuwafuatia ndugu zao?