Naye Absalomu akamwambia Hushai, Je! Huu ndio wema wako kwa rafiki yako? Mbona hukutoka pamoja na rafiki yako?
2 Samueli 16:18 - Swahili Revised Union Version Hushai akamwambia Absalomu, La, sivyo; lakini yule aliyechaguliwa na BWANA, na watu hawa, na watu wote wa Israeli, mimi nitakuwa wake, na pamoja naye nitakaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hushai akamjibu, “La! Maana yule ambaye amechaguliwa na Mwenyezi-Mungu, watu hawa na watu wote wa Israeli, huyo ndiye, mimi nitakuwa wake yeye, na nitabaki naye. Biblia Habari Njema - BHND Hushai akamjibu, “La! Maana yule ambaye amechaguliwa na Mwenyezi-Mungu, watu hawa na watu wote wa Israeli, huyo ndiye, mimi nitakuwa wake yeye, na nitabaki naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hushai akamjibu, “La! Maana yule ambaye amechaguliwa na Mwenyezi-Mungu, watu hawa na watu wote wa Israeli, huyo ndiye, mimi nitakuwa wake yeye, na nitabaki naye. Neno: Bibilia Takatifu Hushai akamwambia Absalomu, “La hasha! Yeye aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu, aliyechaguliwa na watu hawa, atakayechaguliwa tena na wanaume wote wa Israeli, huyu ndiye nitakayekuwa wake, nami nitabakia pamoja naye. Neno: Maandiko Matakatifu Hushai akamwambia Absalomu, “La hasha, yeye aliyechaguliwa na bwana, aliyechaguliwa na watu hawa, atakayechaguliwa tena na watu wote wa Israeli, huyu ndiye nitakayekuwa wake, nami nitabakia pamoja naye. BIBLIA KISWAHILI Hushai akamwambia Absalomu, La, sivyo; lakini yule aliyechaguliwa na BWANA, na watu hawa, na watu wote wa Israeli, mimi nitakuwa wake, na pamoja naye nitakaa. |
Naye Absalomu akamwambia Hushai, Je! Huu ndio wema wako kwa rafiki yako? Mbona hukutoka pamoja na rafiki yako?
Na tena, Ni nani ambaye yanipasa nimtumikie? Hainipasi kumtumikia mwanawe? Kama nilivyomtumikia baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mbele yako.
Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na Roho ya BWANA ikamjia Daudi kwa nguvu kuanzia siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.