Lakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamlazimisha, akalala naye.
2 Samueli 13:15 - Swahili Revised Union Version Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, Amnoni akamchukia Tamari kupita kiasi. Akamchukia Tamari kuliko alivyompenda hapo awali. Akamwambia Tamari, “Ondoka mara moja.” Biblia Habari Njema - BHND Kisha, Amnoni akamchukia Tamari kupita kiasi. Akamchukia Tamari kuliko alivyompenda hapo awali. Akamwambia Tamari, “Ondoka mara moja.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, Amnoni akamchukia Tamari kupita kiasi. Akamchukia Tamari kuliko alivyompenda hapo awali. Akamwambia Tamari, “Ondoka mara moja.” Neno: Bibilia Takatifu Kisha Amnoni akamchukia Tamari, kwa machukio makuu sana. Kwa kweli, Amnoni alimchukia kuliko alivyokuwa amempenda. Amnoni akamwambia, “Inuka na utoke nje!” Neno: Maandiko Matakatifu Kisha Amnoni akamchukia Tamari, kwa machukio makuu sana. Kwa kweli, Amnoni alimchukia kuliko alivyokuwa amempenda. Amnoni akamwambia, “Inuka na utoke nje!” BIBLIA KISWAHILI Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. |
Lakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamlazimisha, akalala naye.
Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunifukuza ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza.
Na watu wa Babeli wakamwendea katika kitanda cha mapenzi, wakamtia unajisi kwa uzinzi wao, akatiwa unajisi nao, kisha roho yake ikafarakana nao.