Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
2 Samueli 1:8 - Swahili Revised Union Version Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema yeye aliniuliza mimi ni nani, nami nikamwambia kuwa mimi ni Mmaleki. Biblia Habari Njema - BHND yeye aliniuliza mimi ni nani, nami nikamwambia kuwa mimi ni Mmaleki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza yeye aliniuliza mimi ni nani, nami nikamwambia kuwa mimi ni Mmaleki. Neno: Bibilia Takatifu “Akaniuliza, ‘Wewe ni nani?’ “Nikamjibu, ‘Mimi ni Mwamaleki.’ Neno: Maandiko Matakatifu “Akaniuliza, ‘Wewe ni nani?’ “Nikamjibu, ‘Mimi ni Mwamaleki.’ BIBLIA KISWAHILI Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki. |
Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Unatoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.
Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu.
Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema, Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa; Lakini mwisho wake atapata uharibifu.
Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.
Naye Daudi na watu wake walikuwa wakikwea na kuwashambulia Wageshuri, na Wagirizi, na Waamaleki waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo, tangu Telemu, hapo uendapo Shuri, mpaka nchi ya Misri.
Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto;
Ndipo Daudi akamwuliza, Wewe ni mtu wa nani; na umetoka wapi? Naye akasema, Mimi ni kijana wa Misri, mtumishi wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu tangu siku hizi tatu nilishikwa na ugonjwa.
Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hadi jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia.