Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
1 Yohana 5:21 - Swahili Revised Union Version Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu kutoka kwa sanamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu! Biblia Habari Njema - BHND Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu! Neno: Bibilia Takatifu Watoto wapendwa, jilindeni nafsi zenu kutokana na sanamu. Amen. Neno: Maandiko Matakatifu Watoto wapendwa, jilindeni nafsi zenu kutokana na sanamu. Amen. BIBLIA KISWAHILI Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. |
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli;
Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
Na wanadamu waliobakia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kutembea.