Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.
1 Wakorintho 15:51 - Swahili Revised Union Version Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikilizeni, nawaambieni siri: Sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa, Biblia Habari Njema - BHND Sikilizeni, nawaambieni siri: Sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikilizeni, nawaambieni siri: sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa, Neno: Bibilia Takatifu Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa: Neno: Maandiko Matakatifu Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa BIBLIA KISWAHILI Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, |
Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.
baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;
bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twapumua kwa shida, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, kulingana na radhi yake aliyoikusudia katika yeye huyo.
ya kwamba kwa kufunuliwa nilijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.
atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.