Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




1 Wafalme 8:51 - Swahili Revised Union Version

Kwa kuwa ni watu wako, na urithi wako, uliowatoa katika Misri, toka katikati ya tanuri ya chuma.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

maana ni watu wako, na ni mali yako; watu ambao uliwatoa Misri kutoka katika tanuri ya chuma.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

maana ni watu wako, na ni mali yako; watu ambao uliwatoa Misri kutoka katika tanuri ya chuma.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

maana ni watu wako, na ni mali yako; watu ambao uliwatoa Misri kutoka katika tanuri ya chuma.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

kwa maana ni watu wako na urithi wako, uliowatoa Misri, kutoka lile tanuru la kuyeyushia chuma.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

kwa maana ni watu wako na urithi wako, uliowatoa Misri, kutoka kwenye lile tanuru la kuyeyushia chuma.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa kuwa ni watu wako, na urithi wako, uliowatoa kutoka Misri, toka katikati ya tanuri ya chuma.

Tazama sura
Tafsiri zingine



1 Wafalme 8:51
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana uliwatenga na watu wote wa dunia, wawe urithi wako, kama ulivyonena kwa mdomo wa Musa, mtumishi wako, hapo ulipowatoa baba zetu katika Misri, Ee Bwana MUNGU.


basi uyasikie toka mbinguni, toka makaoni mwako, wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao; ukawasamehe watu wako, waliokosa juu yako.


Basi watu hao ni watumishi wako na watu wako, uliowakomboa kwa uweza wako mwingi, na kwa mkono wako hodari.


Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge, uwachukue milele.


Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuri ya mateso.


Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.


Niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuri ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;


Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.


Kisha Nebukadneza akaukaribia mlango wa lile tanuri lililokuwa linawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto.


Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.


Bali BWANA amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuri ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo hivi leo.