Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa machimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma chochote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.
1 Wafalme 6:8 - Swahili Revised Union Version Mlango wa vyumba vya chini ulikuwapo upande wa kulia wa nyumba; mtu hupanda ngazi za kuzunguka mpaka vyumba vya katikati, na kutoka vile vya katikati mpaka vile vya tatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mlango wa kuingilia sehemu ya chini ya jengo lililoongezwa ubavuni mwa nyumba, ulikuwa upande wa kusini. Ndani, mlikuwa na ngazi ambayo watu waliweza kupanda ili kwenda ghorofa ya katikati na ya mwisho. Biblia Habari Njema - BHND Mlango wa kuingilia sehemu ya chini ya jengo lililoongezwa ubavuni mwa nyumba, ulikuwa upande wa kusini. Ndani, mlikuwa na ngazi ambayo watu waliweza kupanda ili kwenda ghorofa ya katikati na ya mwisho. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mlango wa kuingilia sehemu ya chini ya jengo lililoongezwa ubavuni mwa nyumba, ulikuwa upande wa kusini. Ndani, mlikuwa na ngazi ambayo watu waliweza kupanda ili kwenda ghorofa ya katikati na ya mwisho. Neno: Bibilia Takatifu Ingilio la ghorofa ya chini kabisa lilikuwa upande wa kusini wa Hekalu; ngazi ilielekea ghorofa ya kati na kutoka hapo ilielekea hadi ghorofa ya tatu. Neno: Maandiko Matakatifu Ingilio la ghorofa ya chini kabisa lilikuwa upande wa kusini wa Hekalu, ngazi ilielekea ghorofa ya kati na kutokea hapo ilielekea hadi ghorofa ya tatu. BIBLIA KISWAHILI Mlango wa vyumba vya chini ulikuwapo upande wa kulia wa nyumba; mtu hupanda ngazi za kuzunguka mpaka vyumba vya katikati, na kutoka vile vya katikati mpaka vile vya tatu. |
Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa machimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma chochote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.
Basi ndivyo alivyoijenga nyumba, akaimaliza; akaifunika nyumba kwa boriti na mbao za mwerezi.
Nenda nyumbani kwa Warekabi, ukanene nao, ukawalete nyumbani kwa BWANA, katika chumba kimoja, ukawape divai wanywe.
Maana vilikuwa vina ghorofa tatu, wala havikuwa na nguzo kama nguzo za zile nyua; basi kila kilichokuwa cha juu kilikuwa chembamba kuliko cha chini na cha katikati, kutoka chini.