Yuda ni mwanasimba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha?
1 Wafalme 10:20 - Swahili Revised Union Version Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya ngazi sita huku na huko; wala hakikufanyika kwa mkono wake katika ufalme wowote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kulikuwa pia na sanamu kumi na mbili za simba zimesimama, moja mwishoni mwa kila ngazi. Kiti kama hicho hakijawahi kutengenezwa katika ufalme wowote ule. Biblia Habari Njema - BHND Kulikuwa pia na sanamu kumi na mbili za simba zimesimama, moja mwishoni mwa kila ngazi. Kiti kama hicho hakijawahi kutengenezwa katika ufalme wowote ule. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kulikuwa pia na sanamu kumi na mbili za simba zimesimama, moja mwishoni mwa kila ngazi. Kiti kama hicho hakijawahi kutengenezwa katika ufalme wowote ule. Neno: Bibilia Takatifu Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kiti kama hicho kiliwahi kutengenezwa katika ufalme mwingine wowote. Neno: Maandiko Matakatifu Simba kumi na wawili walisimama kwenye ngazi sita, mmoja katika kila upande wa kila ngazi. Hakuna kitu kama hicho kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme mwingine wowote. BIBLIA KISWAHILI Na simba kumi na wawili wamesimama juu ya ngazi sita huku na huko; wala hakikufanyika kwa mkono wake katika ufalme wowote. |
Yuda ni mwanasimba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha?
Kiti kile kilikuwa na ngazi sita, na juu yake kimeviringana nyuma; na mikono huku na huko mahali pa kuketi, na simba wawili wakisimama kando ya hiyo mikono.
Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.
Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba jike, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hadi atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.
Aliinama, akalala mfano wa simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha? Na abarikiwe kila akubarikiye, Na alaaniwe kila akulaaniye.
Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na ile mihuri yake saba.