Naye mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, kila alilotaka, zaidi ya hayo aliyopewa na Sulemani kwa ukarimu wake wa kifalme. Basi, akarudi akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
1 Wafalme 10:14 - Swahili Revised Union Version Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani mwaka mmoja, ndio talanta mia sita sitini na sita, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila mwaka, Solomoni alipelekewa dhahabu kilo 22,000. Biblia Habari Njema - BHND Kila mwaka, Solomoni alipelekewa dhahabu kilo 22,000. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila mwaka, Solomoni alipelekewa dhahabu kilo 22,000. Neno: Bibilia Takatifu Uzito wa dhahabu ambayo Sulemani alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta mia sita sitini na sita (666), Neno: Maandiko Matakatifu Uzito wa dhahabu ambayo Sulemani alipokea kwa mwaka ulikuwa talanta 666, BIBLIA KISWAHILI Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Sulemani mwaka mmoja, ndio talanta mia sita sitini na sita, |
Naye mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba haja yake yote, kila alilotaka, zaidi ya hayo aliyopewa na Sulemani kwa ukarimu wake wa kifalme. Basi, akarudi akaenda zake katika nchi yake, yeye na watumishi wake.
Na mambo yale usiyoyaomba nimekupa, mali na fahari, hata hapatakuwa na mtu katika wafalme kama wewe, siku zako zote.
Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.
tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, wanaume kwa wanawake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana.