mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake; msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nikija nitayatengeneza.
1 Timotheo 3:14 - Swahili Revised Union Version Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ninakuandikia barua hii nikiwa na matumaini ya kuja kwako hivi karibuni. Biblia Habari Njema - BHND Ninakuandikia barua hii nikiwa na matumaini ya kuja kwako hivi karibuni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ninakuandikia barua hii nikiwa na matumaini ya kuja kwako hivi karibuni. Neno: Bibilia Takatifu Ingawa ninatarajia kuja kwako hivi karibuni, ninakuandikia maagizo haya sasa ili, Neno: Maandiko Matakatifu Ingawa ninatarajia kuja kwako hivi karibuni, ninakuandikia maagizo haya sasa ili kwamba, BIBLIA KISWAHILI Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu. |
mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake; msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nikija nitayatengeneza.
Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, nilitaka kuja mara kwa mara, lakini Shetani akatuzuia.
Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana natumaini ya kwamba kwa maombi yenu nitarejeshwa kwenu.
Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye.
Kwa kuwa ninayo mambo mengi, sitaki kuyaandika kwa karatasi na wino; lakini natarajia kuja kwenu, na kusema nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu iwe imetimizwa.