Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa miungu yao, wakakitundika kichwa chake nyumbani mwa Dagoni.
1 Samueli 5:2 - Swahili Revised Union Version Wafilisti wakalichukua sanduku la Mungu, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, wakalipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu kwenye hekalu la mungu wao Dagoni na kuliweka karibu naye. Biblia Habari Njema - BHND Kisha, wakalipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu kwenye hekalu la mungu wao Dagoni na kuliweka karibu naye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, wakalipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu kwenye hekalu la mungu wao Dagoni na kuliweka karibu naye. Neno: Bibilia Takatifu Kisha wakaliingiza lile Sanduku ndani ya hekalu la Dagoni na kuliweka kando ya huyo Dagoni. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha wakaliingiza lile Sanduku ndani ya hekalu la Dagoni na kuliweka kando ya huyo Dagoni. BIBLIA KISWAHILI Wafilisti wakalichukua sanduku la Mungu, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni. |
Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa miungu yao, wakakitundika kichwa chake nyumbani mwa Dagoni.
Hata ikawa siku ya pili yake Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara hao waliouawa, walimwona Sauli na wanawe wameanguka juu ya mlima Gilboa.
Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile vyombo vya dhahabu na fedha, ambavyo baba yake, Nebukadneza, alivitoa katika hekalu lililokuwako Yerusalemu; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na masuria wake, wapate kuvinywea.
Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lolote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.
Kisha atapita kwa kasi, kama upepo, atapita na kuwa ana hatia; yeye ambaye nguvu zake ni mungu wake.
Kwa sababu hiyo huutolea wavu wake sadaka, na kulifukizia uvumba juya lake; kwa sababu kwa vitu vile fungu lake limenona, na chakula chake kimekuwa tele.
Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.