Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
1 Samueli 4:19 - Swahili Revised Union Version Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja mzito, karibu ajifungue; basi, aliposikia kuhusu kutwaliwa kwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha na kujifungua; maana uchungu wake ulimfikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena ilitokea kwamba, mkwewe Eli, yaani mke wa Finehasi, wakati huo alikuwa mjamzito, na muda wake wa kujifungua ulikuwa umekaribia. Aliposikia kwamba sanduku la agano la Mungu limetekwa na kwamba baba mkwe wake, hata na mumewe wamefariki, mara moja alipata utungu, na kujifungua. Biblia Habari Njema - BHND Tena ilitokea kwamba, mkwewe Eli, yaani mke wa Finehasi, wakati huo alikuwa mjamzito, na muda wake wa kujifungua ulikuwa umekaribia. Aliposikia kwamba sanduku la agano la Mungu limetekwa na kwamba baba mkwe wake, hata na mumewe wamefariki, mara moja alipata utungu, na kujifungua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena ilitokea kwamba, mkwewe Eli, yaani mke wa Finehasi, wakati huo alikuwa mjamzito, na muda wake wa kujifungua ulikuwa umekaribia. Aliposikia kwamba sanduku la agano la Mungu limetekwa na kwamba baba mkwe wake, hata na mumewe wamefariki, mara moja alipata utungu, na kujifungua. Neno: Bibilia Takatifu Mkwewe, mke wa Finehasi, alikuwa mjamzito na alikaribia wakati wa kujifungua. Aliposikia habari kwamba Sanduku la Mungu limetekwa na ya kuwa baba mkwe wake na mumewe wamekufa, akapata uchungu naye akajifungua lakini akazidiwa na uchungu. Neno: Maandiko Matakatifu Mkwewe, mke wa Finehasi, alikuwa mjamzito na karibu wakati wa kujifungua. Aliposikia habari kwamba Sanduku la Mungu limetekwa na ya kuwa baba mkwe wake na mumewe wamekufa, akapata utungu naye akajifungua lakini akazidiwa na utungu. BIBLIA KISWAHILI Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja mzito, karibu ajifungue; basi, aliposikia kuhusu kutwaliwa kwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha na kujifungua; maana uchungu wake ulimfikia. |
Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Ikawa alipokuwa anashikwa sana na uchungu, mkunga akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine.
basi, nitafanya nyumba hii kuwa kama Shilo, na mji huu nitaufanya kuwa laana kwa mataifa yote ya dunia.
Ikawa alipolitaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye alikuwa amewaamua Waisraeli miaka arubaini.
Na alipokuwa karibu kufa, wale wanawake waliokuwa wakimuhudumia wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto wa kiume. Lakini hakujibu, wala hakumtazama.