Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake.
1 Samueli 24:21 - Swahili Revised Union Version Basi sasa, uniapie kwa BWANA, ya kwamba hutawakatilia mbali wazao wangu baada yangu, wala hutaliharibu jina langu katika ukoo wa baba yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini niapie kwa jina la Mwenyezi-Mungu kuwa hutawakatilia mbali wazawa wangu, wala kufutilia mbali jina langu katika jamaa ya baba yangu.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini niapie kwa jina la Mwenyezi-Mungu kuwa hutawakatilia mbali wazawa wangu, wala kufutilia mbali jina langu katika jamaa ya baba yangu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini niapie kwa jina la Mwenyezi-Mungu kuwa hutawakatilia mbali wazawa wangu, wala kufutilia mbali jina langu katika jamaa ya baba yangu.” Neno: Bibilia Takatifu Sasa niapie kwa Mwenyezi Mungu kwamba hutakatilia mbali uzao wangu wala kulifuta jina langu kutoka jamaa ya baba yangu.” Neno: Maandiko Matakatifu Sasa niapie kwa bwana kwamba hutakatilia mbali uzao wangu wala kulifuta jina langu kutoka jamaa ya baba yangu.” BIBLIA KISWAHILI Basi sasa, uniapie kwa BWANA, ya kwamba hutawakatilia mbali wazao wangu baada yangu, wala hutaliharibu jina langu katika ukoo wa baba yangu. |
Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake.
Labani akasema, Chungu hii ni shahidi kati ya mimi na wewe hivi leo. Kwa hiyo likaitwa jina lake Galedi,
Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu. Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake.
Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao mwisho wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha.
Akamwambia, Usiogope, kwa maana mkono wa Sauli, babangu, hautakupata; na wewe utakuwa mfalme juu ya Israeli; na mimi nitakuwa makamu wako; ndivyo ajuavyo hata Sauli, babangu.
Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika BWANA atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya BWANA; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.
Tena itakuwa, hapo BWANA atakapokuwa amemtendea bwana wangu sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli;