Basi wakageuka wakaenda kuko, wakafika katika nyumba ya huyo kijana Mlawi, huko nyumbani kwa Mika, kumwamkia.
1 Samueli 10:4 - Swahili Revised Union Version nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Watakusalimia na kukupa mikate miwili, nawe utaipokea mikononi mwao. Biblia Habari Njema - BHND “Watakusalimia na kukupa mikate miwili, nawe utaipokea mikononi mwao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Watakusalimia na kukupa mikate miwili, nawe utaipokea mikononi mwao. Neno: Bibilia Takatifu Watakusalimu na kukupa mikate miwili, ambayo utaipokea kutoka kwao. Neno: Maandiko Matakatifu Watakusalimu na kukupa mikate miwili, ambayo utaipokea kutoka kwao. BIBLIA KISWAHILI nao watakusalimu na kukupa mikate miwili; nawe utaipokea mikononi mwao. |
Basi wakageuka wakaenda kuko, wakafika katika nyumba ya huyo kijana Mlawi, huko nyumbani kwa Mika, kumwamkia.
Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na kufika kwenye mwaloni wa Tabori, na hapo watu watatu watakutana nawe, wanaokwea kumwendea Mungu huko Betheli, mmoja anachukua wana-mbuzi watatu, na mwingine anachukua mikate mitatu, na mwingine anachukua kiriba cha divai;
Baada ya hayo utafika Gibea ya Mungu, hapo palipo na ngome ya Wafilisti; kisha itakuwa, utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakishuka kutoka mahali pa juu, wenye kinanda, na tari, na kinubi, na filimbi mbele yao, nao watakuwa wakitabiri;
Yese akatwaa punda, wa kuchukua mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, akampelekea Sauli kwa mkono wa Daudi mwanawe.