Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
1 Petro 1:9 - Swahili Revised Union Version katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani yenu. Biblia Habari Njema - BHND kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani yenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani yenu. Neno: Bibilia Takatifu Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu. Neno: Maandiko Matakatifu Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu. BIBLIA KISWAHILI katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. |
Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
Hawa wote wakafa katika imani, walikuwa hawajazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.
Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
watu wasiotii hapo zamani, wakati Mungu alipowavumilia kwa subira, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.