Zekaria 6:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao walio mbali watakuja na kusaidia kujenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Watu wanaokaa nchi za mbali watakuja kusaidia kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.” Nanyi mtajua kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Biblia Habari Njema - BHND “Watu wanaokaa nchi za mbali watakuja kusaidia kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.” Nanyi mtajua kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Watu wanaokaa nchi za mbali watakuja kusaidia kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.” Nanyi mtajua kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Neno: Bibilia Takatifu Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la Mwenyezi Mungu, nanyi mtajua kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa bidii.” Neno: Maandiko Matakatifu Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la bwana, nanyi mtajua ya kwamba bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa bidii.” BIBLIA KISWAHILI Nao walio mbali watakuja na kusaidia kujenga hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu. |
Tazama, hawa watakuja kutoka mbali; na tazama, hawa kutoka kaskazini, na kutoka magharibi, na hawa kutoka nchi ya Sinimu.
Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.
Na wageni watajenga kuta zako, Na wafalme wao watakuhudumu; Maana katika ghadhabu yangu nilikupiga, Lakini katika upendeleo wangu nimekurehemu.
lakini niliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru mpate kufanikiwa.
Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.
BWANA wa majeshi asema hivi, Ikiwa utaenda katika njia zangu, na kushika maagizo yangu, basi utaihukumu nyumba yangu, na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa haki ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.
ukamwambie, ukisema, BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni Chipukizi; naye atakua katika mahali pake, naye atalijenga hekalu la BWANA.
Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.
ukiwa utaifuata sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa kuyashika maagizo yake, na amri zake zilizoandikwa katika kitabu hiki cha torati; ukimwelekea BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote.