Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, na wanaomwudhi, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku.
Zekaria 12:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitayaangamiza mataifa yote yatakayokuja kupigana na Yerusalemu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Siku hiyo, nitayaangamiza mataifa yote yanayotaka kuushambulia mji wa Yerusalemu. Biblia Habari Njema - BHND “Siku hiyo, nitayaangamiza mataifa yote yanayotaka kuushambulia mji wa Yerusalemu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Siku hiyo, nitayaangamiza mataifa yote yanayotaka kuushambulia mji wa Yerusalemu. Neno: Bibilia Takatifu Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu. BIBLIA KISWAHILI Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitayaangamiza mataifa yote yatakayokuja kupigana na Yerusalemu. |
Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, na wanaomwudhi, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku.
Tazama, hakika ikiwa utashambuliwa na yeyote, haitakuwa kwa shauri langu. Yeyote atakayekushambulia ataanguka kwa ajili yako.
Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.
nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake.
Angalia, mimi nitafanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbayumba kwa watu wa kabila zote, wazungukao pande zote; tena kitakuwa juu ya Yuda pia wakati wa kuhusuriwa Yerusalemu.