Zekaria 11:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA akaniambia, Jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akaniambia tena, “Jifanye tena mchungaji, lakini safari hii uwe kama mchungaji mbaya! Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akaniambia tena, “Jifanye tena mchungaji, lakini safari hii uwe kama mchungaji mbaya! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akaniambia tena, “Jifanye tena mchungaji, lakini safari hii uwe kama mchungaji mbaya! Neno: Bibilia Takatifu Kisha Mwenyezi Mungu akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha bwana akaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu. BIBLIA KISWAHILI BWANA akaniambia, Jitwalie tena vyombo vya mchungaji mpumbavu. |
Manabii wako wameona maono kwa ajili yako Ya ubatili na upumbavu Wala hawakufunua uovu wako, Wapate kurudisha kufungwa kwako; Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako Na sababu za kuhamishwa.
Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao manabii wajinga, wanaoifuata roho yao wenyewe, wala hawakuona neno lolote!
Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kulia; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kulia litakuwa limepofuka.
Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.
Wapumbavu ninyi na vipofu; maana ni ipi iliyo kubwa, ile dhahabu, au lile hekalu liitakasalo dhahabu?