Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
Zekaria 1:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kisha BWANA akanionesha wafua chuma wanne. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, Mwenyezi-Mungu akanionesha wafuachuma wanne. Biblia Habari Njema - BHND Kisha, Mwenyezi-Mungu akanionesha wafuachuma wanne. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, Mwenyezi-Mungu akanionesha wafuachuma wanne. Neno: Bibilia Takatifu Kisha Mwenyezi Mungu akanionesha mafundi wanne. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha bwana akanionyesha mafundi wanne. BIBLIA KISWAHILI Kisha BWANA akanionesha wafua chuma wanne. |
Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa kutoka mikononi mwa adui zao.
Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kazi kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia.
Tena waokoaji watakwea juu ya mlima Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya BWANA.
Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.
lakini hapo walipokwea kutoka Misri, na Israeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu, na Kadeshi;
Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki mwa nchi ya Moabu, wakapiga kambi upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.
BWANA akawatuma Yerubaali, na Baraka, na Yeftha, na Samweli, akawaokoa ninyi kutoka kwa mikono ya adui zenu pande zote, nanyi mkakaa salama.