Zaburi 99:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; abuduni katika mlima wake mtakatifu! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu. Biblia Habari Njema - BHND Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; abuduni katika mlima wake mtakatifu! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msifuni Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; abuduni katika mlima wake mtakatifu! Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu. Neno: Bibilia Takatifu Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ni mtakatifu. Neno: Maandiko Matakatifu Mtukuzeni bwana Mwenyezi Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana bwana Mwenyezi Mungu wetu ni mtakatifu. BIBLIA KISWAHILI Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu. |
bali BWANA wa majeshi ametukuzwa katika hukumu, na Mungu aliye Mtakatifu ametakaswa katika haki.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
Ee BWANA, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee BWANA, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe.
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna yeyote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.