Zaburi 99:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akasema nao katika nguzo ya wingu. Wakashika shuhuda zake na amri aliyowapa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alisema nao katika mnara wa wingu; waliyazingatia matakwa yake na amri alizowapa. Biblia Habari Njema - BHND Alisema nao katika mnara wa wingu; waliyazingatia matakwa yake na amri alizowapa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alisema nao katika mnara wa wingu; waliyazingatia matakwa yake na amri alizowapa. Neno: Bibilia Takatifu Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa. Neno: Maandiko Matakatifu Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa. BIBLIA KISWAHILI Akasema nao katika nguzo ya wingu. Wakashika shuhuda zake na amri aliyowapa. |
BWANA akamwambia Musa, Tazama, mimi naja kwako katika wingu zito ili watu hawa wasikie nitakaposema nawe, nao wapate kukuamini nawe hata milele. Musa akamwambia BWANA hayo maneno ya watu.
Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema; naye BWANA akasema na Musa.
BWANA akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.
Musa akakasirika sana, akamwambia BWANA. Usiikubali sadaka yao; mimi sikutwaa hata punda mmoja kwao, wala sikumwumiza hata mtu mmoja miongoni mwao.
Aliyemtaja baba yake na mama yake, Mimi sikumwona; Wala nduguze hakuwakubali; Wala hakuwajua watoto wake mwenyewe; Maana wameliangalia neno lako, Wamelishika agano lako.
Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.
aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.