Ingieni malangoni mwake kwa shukrani; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
Zaburi 96:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mpeni BWANA utukufu wa jina lake, Leteni sadaka, na mwingie katika nyua zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lisifuni jina lake tukufu; leteni tambiko na kuingia hekaluni mwake. Biblia Habari Njema - BHND Lisifuni jina lake tukufu; leteni tambiko na kuingia hekaluni mwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lisifuni jina lake tukufu; leteni tambiko na kuingia hekaluni mwake. Neno: Bibilia Takatifu Mpeni Mwenyezi Mungu utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. Neno: Maandiko Matakatifu Mpeni bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. BIBLIA KISWAHILI Mpeni BWANA utukufu wa jina lake, Leteni sadaka, na mwingie katika nyua zake. |
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
Watu wa nchi nao wataabudu mbele ya mlango wa lile lango mbele za BWANA, siku za sabato, na siku za mwezi mwandamo.
Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.
Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.
Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.
Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa muwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.