Zaburi 96:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Furahini enyi mbingu na dunia! Bahari na ivume pamoja na vyote vilivyomo! Biblia Habari Njema - BHND Furahini enyi mbingu na dunia! Bahari na ivume pamoja na vyote vilivyomo! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Furahini enyi mbingu na dunia! Bahari na ivume pamoja na vyote vilivyomo! Neno: Bibilia Takatifu Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyo ndani yake; Neno: Maandiko Matakatifu Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; BIBLIA KISWAHILI Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, Bahari na ivume na vyote viijazavyo, |
Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.
Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.
Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.