Zaburi 92:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa umenifurahisha, BWANA, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, matendo yako yanifurahisha; nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, matendo yako yanifurahisha; nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, matendo yako yanifurahisha; nitashangilia kwa sababu ya mambo yote uliyotenda. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, kwa kuwa matendo yako yamenifurahisha, nitaziimba kwa shangwe kazi za mikono yako. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa umenifurahisha, BWANA, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako. |
Nimezikumbuka siku za kale, Nimeyatafakari matendo yako yote, Naziwaza kazi za mikono yako.
Maana BWANA asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee BWANA, uwaokoe watu wako, mabaki ya Israeli.
Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.
Ila Mungu ashukuriwe, anayetufanya tushangilie ushindi daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.