Zaburi 92:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema huendelea kuzaa matunda hata uzeeni; daima wamejaa utomvu na wabichi; Biblia Habari Njema - BHND huendelea kuzaa matunda hata uzeeni; daima wamejaa utomvu na wabichi; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza huendelea kuzaa matunda hata uzeeni; daima wamejaa utomvu na wabichi; Neno: Bibilia Takatifu Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu, Neno: Maandiko Matakatifu Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu, BIBLIA KISWAHILI Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. |
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.
Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.
Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa joto ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.
Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayataisha kamwe; utatoa matunda mapya kila mwezi, kwa sababu maji yake yanatoka mahali patakatifu; na matunda yake yatakuwa ni chakula; na majani yake yatakuwa ni dawa.
Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Watu hawa ni miamba yenye hatari katika karamu zenu za upendo walapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo hofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa mara mbili, na kung'olewa kabisa;